![]() |
Kikosi cha Simba kilichotwaa ubingwa leo kikiwa kambini Zanzibar, baada ya Mtibwa Sugar kuituliza Azam kwa kichapo cha mabao 2-1. |
SIMBA
leo wanaanza kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
baada ya Azam FC kufungwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Simba
ina pointi 59, ambazo sasa haziwezi kufikiwa na timu yoyote msimu huu
na imebakiza mechi moja dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumapili ambayo
kwao itakuwa ya kulinda heshima tu.
Lakini
Azam tayari imejihakikishia nafasi ya pili kwenye ligi hiyo na hivyo
kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
Waliokuwa
mabingwa watetezi Yanga, hawana tena chao- kwani hata wakiifunga Simba
keshokutwa watabaki nafasi ya tatu tu, hivyo mwakani hawavuki mipaka ya
nchi.
Tumaini
pekee la Yanga kucheza michuano ya Afrika mwakani ni iwapo Simba SC
itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu- ikiwa
imebakiza mitihani miwili kufikia mafanikio hayo.
Inatakiwa
kuitoa Al Ahly Shandy ya Sudan- na baadaye iitoe timu itakayokutana
nayo kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua hiuyo, ambayo itakuwa
imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.
Hapo,
Tanzania itakuwa na nafasi mbili kwenye Kombe la Shirikisho mwakani,
kwa mujibu wa kanuni mpya za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Tayari
Simba imeifunga Shandy mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza na inahitaji
sare katika mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kusonga mbele.
Katika
mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa
bao 1-0 lililowekwa kimiani na Awadh Issa dakika ya 25, wakati kipindi
cha pili, Wakata Miwa hao wa Manungu waliokuwa wanashangiliwa kwa nguvu
na mashabiki wa Simba, walipata bao la pili dakika ya 59, mfungaji akiwa
ni Juma Abdul.
Awadh alifunga bao lake akiunganisha kona iliyochongwa na nyota wa mchezo wa leo, Juma Abdul ambaye naye alifunga bao
la pili kwa mpira wa adhabu, baada ya Luckson Kakolaki kumchezea rafu
Vencent Barnabas Saramba. John Raphael Bocco aliifungia Azam bao la
kufutia machozi.
SOURCE: BIN ZUBEIRY (http/bongostaz.blogspot.com na http://mamapipiro.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment