skip to main |
skip to sidebar

5/14/2012 07:26:00 AM

Unknown
No comments

SIMBA SC imeshindwa kutimiza ndoto za kusonga mbele kwenye Kombe la
Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kutolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly
Shandy ya Sudan kufuatia sare ya jumla ya tatu.
Katika mchezo huo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shandi, penalti za
Shandy zilifungwa na Razak Yakubu, Orwa, Bashir, Saddam, Isaac Seun
Malik, Faris Abdallah, Fareed Mohamed Zakaria Nasu na kipa Abdulrahman
Ali.
Waliofunga penalti za Simba ni Felix Sunzu, Salum Machaku, Emanuel Okwi,
Shomari Kapombe, Kelvin Yondan, Victor Costa, Mwinyi Kazimoto na Amir
Maftah.
Eltigani alikosa kwa upande wa Shandy wakati Mafisango na Kaseja
walikosa. Aliyeihakikishia Simba kutolewa alikuwa ni Nahodha Kaseja,
ambaye alikosa penalti ya 10.
Shandy waliingia kwenye mchezo wa leo, wakiwa nyuma kwa 3-0 kutokana na
ujshindi wa SImba kwenye mechi ya kwanza, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake na hiyo
ilijenga matumaini kwamba, Simba itasonga mbele, lakini kipindi cha pili
mambo yalibadilika mno.
Mabao mawili ya Fareed Mohamed katika za 46 na 64 na lingine la Hamouda
Bashir dakika ya 50, yaliisaidia Al Ahly Shandy kushinda 3-0 na kufanya
sare ya jumla ya 3-3, baada ya dakika 180 za mechi mbili.
Lawama zote zimuendee beki Victor Costa kwa kufungisha mabao mawili-
hususani la pili na la tatu ambalo dhahiri yalitokana na ‘ubishoo’ wake
usio na maana.
Hii inahidhirisha mchezaji huyo aliyepangwa kwa dharula leo, kocha
Milovan Cirkovick alikuwa hakosei kutompanga- kwani leo ameigharimu timu
na haijulikani kwa nini apangwe yeye badala ya Obadia Mungusa.
0 comments:
Post a Comment