MUDA
mfupi kabla ya kikosi cha Simba kuondoka mchana wa leo kwenda Tanga kwa
ajili ya mchezo wao wa ligi kuu Bara dhidi ya wenyeji Coastal, idadi ya
wachezaji watakaokosa mchezo huo imeongezeka baada ya mshambulijia wa
timu hiyo Mrisho Ngasa.
Awali,
ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema Ngasa ambaye alikuwa na
Malaria amepona na atakuwwemo katika safari ya Tanga lakini baada ya
daktari wa timu hiyo kuwafanyia vipimo wachezaji kabla ya kuondoka
ilibainika kwamba Ngasa bado ni mgonjwa.
Kamwaga alisema mbali na Ngasa, majeruhi mwingine ni Kigi Makasi ambaye ataungana na haruna Shamte na Komabil Keita .
Aidha,
katika msafara huo pia hatokuwemo mshambuliaji wao Emmanuel Okwi ambaye
amekwenda kwao Uganda kujiunga na timu ya Taifa, huku Abdala Seseme na
Waziri Mahadi wakiachwa kwa sababu za kiufundi.
Makipa
Juma Kaseja, Wilbert Mweta
Walinzi
Chollo, Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema.
VIUNGO
Kazimoto, Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban
Washambuliaji
Sunzu, Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma
0 comments:
Post a Comment