WASANII wa muziki wa kizazi kipya, Linah na Maunda Zorro wanatarajia kumpiga tafu msanii mwenzao, Bayonga Batitoi a.k.a 2.Friends katika nyimbo zake mbili anazotarajia kuzirekodi ‘soon’.
Akipiga soga na Za motomoto juzikati jijini Dar, 2.Friends ambaye ameachia kibao chake kikali kinachoenda kwa jina la ‘Unajifanya Hujui’ alisema, anajua uwezo wa wasanii hao ndiyo maana anakusudia kupiga nao kolabo.
“Natambua uwezo wa wasanii hawa ndiyo maana nimewaomba wanipige tafu ili nyimbo zangu ziwe na ladha tofauti, natarajia kukamilisha albamu hiyo ya nyimbo nane hivi karibuni,” alisema 2.Friends.
0 comments:
Post a Comment