Monday, December 5, 2011

Afya ya Shilole tia maji tia maji


Na Jacob Baraka
AFYA ya staa wa filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) ni tia maji tia maji kwani kwa siku kadhaa amelala kitandani akisumbuliwa na ugonjwa usiokubalika wa malaria.

Akizungumza kwa tabu mbele ya habarizaudaku.co.cc mwishoni mwa wiki iliyopita, Shilole alisema alizidiwa ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi Kinondoni, Dar es Salaam ambapo alilazwa siku nzima na kutundikiwa dripu za maji na dawa baada ya kugundulika kuwa ana malaria kali.

Alisema ugonjwa huo ulimpelekesha vibaya kutokana na kutougua kwa muda mrefu na kutokuwa na tabia ya kucheki afya mara kwa mara.

“Kwa sasa naendelea vizuri, lakini kiukweli hali yangu ilikuwa mbaya,” alisema Shilole na kuwashukuru wasanii wenzake wa Bongo Movie kwa upendo waliouonesha kwake.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine