Monday, December 5, 2011

WEMA TENA HEADLINE KAMA KAWAIDA!!!!




WEMA Isaac Sepetu anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya picha zake akiwa na mwanaume ‘tata’ aliyetajwa kwa jina la Martin kunaswa wakiwa katika pozi za kimahaba.

Sosi ya kuzagaa kwa picha hizo mtandaoni ni mwanaume huyo ambaye alizitundika kwa mara ya kwaza kwenye ‘blogi’ yake huku akielezea hisia zake za kimapenzi kwa mwigizaji huyo ambaye ni mwandani wa mwanamuziki Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’.

Baada ya kuzitundika picha hizo, Martin aliandika: “Nilikutana naye studio (ya kupiga picha). Wema ni mmoja kati ya wasichana wengi ambao nimekutana nao kupitia kazi yangu (umodo).

“Nadhani damu yangu na yake zilipatana na akawa mtu wangu sana. Kiukweli nampenda sana na ana sauti ya kimahaba yaani natamani kumsikiliza muda wote. Nakupenda sana Wema.

“Najisikia raha kumkumbatia, sijui imetokeaje lakini wakati amenikumbatia nilijikuta nimefumba macho, sijui ndiyo utamu wa kukumbatiwa, sijui!

“Nikiambiwa nichague kitu gani binti yangu awe nacho kutoka kwa Wema, nitamchagulia lips (midomo) zake, mtoto ana lips nzuri kichizi, fikiria lips zake zikikunong’oneza kitu masikioni!”

Kwa mujibu wa watu walioziona picha hizo, kwa vyovyote Wema alimtoroka Diamond kwa kuwa mwanamuziki huyo angekuwa naye asingemruhusu kufanya kitendo kama hicho.

Hata hivyo walimalizia kwa kusema: “Ama kweli akiwa ndani ni wako lakini akitoka nje si wako!”


The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Wema ili kufafanua picha hizo simu yake iliita bila kupokelewa lakini hata hivyo, jitihada za kumpata ili afunguke zinaendelea.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine