Thursday, January 12, 2012

HATIMAYE MTIHANI WA KIDATO CHA PILI WAREJESHWA.


Hatimaye ule mtihani wa kidato cha pili uliokuwa umefutwa kwa malengo ya kuwa na wasomi wengi hapa nchini umerejeshwa tena baada ya uchunguzi uliofanywa na baadhi ya watafiti kugundua kuwa kuondolewa kwa mtihani huo hakukuleta madumuni yaliyotarajiwa.Wizara ilitegemea kuwa kuondolewa kwa mtihani huo kungeiwezesha nchi kupata wasomi wengi lakini badala yake kumeanza kujitokeza kwa kundi lisilo na nyuma wala mbele,kwani idadi kubwa ya wanafunzi wanaoferi mtihani wa kidato cha nne imegundulika kuwa wanatokana kwa kuondolewa kwa mtihani huo ambao uliruhusu hata wanafunzi wasiojiweza kusonga mbele na kufikia kidato cha nne.Mtihani huo utaanzwa kufanywa kama kawaida na wanafunzi walio kidato cha pili mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine