Rapper DMX amesema kwamba hamkubali kabisa rapper mwenzake yani Drake, ambapo amesisitiza kwamba hampendi Drake wala hamkubali kwa lolote kuanzia stail yake ya kunyoa, mistari yake, hapendi anachoongea, hapendi sura yake wala hapendi anavyotembea.
Mbali na kummaliza Drake, Dmx pia amemchana Rick Ross kwa kusema hana uhakika kama muziki wake unamvutia.
Amesema anapenda kuzungumzia kuhusu kula tu, sasa atakula kiasi gani? Kingine kinachomkera kuhusu Rick Ross ni kujisifia kuwa na magari ya kifahari na kuimba kuhusu utajiri au mali.
Pamoja na kuwachana marapa hao, Dmx amesema hana tatizo na Lil Wyne, uhusiano wao uko poa ambapo hii ishu imetokea wakati akihojiwa na kituo cha power 105 New York Marekani.
0 comments:
Post a Comment