Saturday, February 25, 2012

NEWSSSSS! KEISHA ARUDI KUFANYA KAZI NA BABTALE WA TIPTOP!

Keisha akiwa on stage
Member wa zamani wa kundi la Tip Top Connection mwimbaji Keisha leo ametangaza kuitoa single yake ya pili kuiandika na kuiimba toka aolewe na kujifungua mtoto ambae ana umri wa zaidi ya mwaka mmoja.
Kingine ambacho kilifanya nishawishike kumuuliza hili swali haraka, ni pale aliposema sasa hivi kwenye hii single anashirikiana kikazi na Meneja wa Tip Top Connection Bab Tale.
Nakumbuka wakati anajitoa TipTop alitangaza kwamba hataki kufanya tena kazi na kundi hilo wala mabosi wake ambao Babtale ni mmoja wapo, lakini nilipomuuliza kamba imekuaje umerudi ulikosema hutorudi alijibu “nadhani watu wamesahau, sikusema sitofanya tena kazi na Babtale, nilisema sitorudi tena kamwe Tiptop Connection, hivyo tu”
Keisha amesema “mambo ya tumbo tuyaweke mbali, sasa hivi tunafanya kazi, tunafanya biashara”

 Stori imeandikwa na MILLARDAYO

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine