NAHODHA wa Timu ya Soka ya taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' Sophia Mwasikili atakuwa huru kucheza soka la kulipwa nchini Uturuki baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutuma hati yake ya uhamisho (ITC). Mwasikili alisimamishwa kuichezea klabu ya Luleburgazgucu Sport inayoshiriki ligi daraja la kwanza baada ya kuchelewa kwa ITC yake ambayo chama cha soka cha Uturuki kilituma maombi ya ITC hiyo TFF. Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema tayari wametuma ITC ya Mwasikili nchini humo hivyo mchezaji huyo atakuwa huru kuendelea kucheza soka la kulipwa nchini humo akiwa na klabu yake hiyo mpya. Tayari tumetuma ITC ya Mwasikili tangu Juzi kama alisimamishwa basi ni tatizo tu la mawasiliano, lakini sasa kila kitu kinakwenda sawa, alisema Wambura na kuongeza kwamba hiyo ni nafasi nzuri kwa mchezaji huyo kusonga mbele katika soka sambamba na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake. |
0 comments:
Post a Comment