Christina Aguilera |
NEW YORK,
MWANAMUZIKI Christina Aguilera amesema wakati umefika wa kumtafuta baba yake mzazi ambaye kwa mara ya mwisho alimwona mwaka 1999.
Aguilera amesema amekusudia kumtafuta baba yake huyo na kutaka wazungumze kwa kuwa amemsamehe kwa mambo aliyomfanyia alipokuwa mdogo.
Nimeshayaanika mabaya yote aliyonifanyia, nafikiri fedheha aliyoipata imetosha kujifunza, nataka nimtafute na tuishi kama baba na mwana ambao hawakuwahi kukoseana,alisema Aguilera.
Hata hivyo anasema mateso aliyopata kwa baba yake aitwaye Fausto yalimfanya akimbilie kwenye muziki ili kujipooza na matokeo yake amepata maisha mazuri.
Baba yake huyo hakuwa baba bora wa familia na alitengana na mama yake Aguilera wakati mwanamuziki huyo alipokuwa na umri wa miaka sita tu.
0 comments:
Post a Comment