Saturday, February 18, 2012

WACHEZAJI WA ZAMBIA KUPEWA MIJENGO

Rasi wa Zambia Michael Sata (mwenye fimbo) akimsaidia kupokea kombe rausi wa kwnza wa nchi hiyo,Kenneth Kaunda (wa tatu kutoka kulia)kutoka kwa nahodha wa Zambia Christopher Katongo baada ya Rais huyo kuwaandalia wachezaji wake chakula cha mchana Ikulu mjini Lusaka
 














LUSAKA, Zambia
TIMU ya Taifa ya Zambia imezidi kuongezewa zawadi baada ya Waziri wa Serikali za Mitaa na Nyumba wa nchi hiyo kukubali wachezaji hao kuwazawadia nyumba kila mchezaji.

Waziri huyo alikubali ombi hilo baada ya kusomwa hotuba na nahodha wa timu ya Taifa ya Zambia, Christopher Katongo kwenye Ikulu ya Zambia na kusema wanahitaji nyumba ukiacha zawadi nyingine wanazopewa.

Tumesikia zawadi mbalimbali tunazohaidiwa kupewa, lakini tulitarajia kusikia pia tutapewa nyumba, alisema Katongo.

Wachezaji wa Zambia walisema hayo juzi wakati walipoandaliwa chakula cha mchana na mke wa raisi wa nchi hiyo katika Ikulu ya Zambia.

Serikali imesikia ombi la wachezaji wa timu ya Taifa ya Zambia na tumelipokea kwa dhati, ila tutafuata utaratibu ili kuhakikisha mnapata hizo nyumba kwa utaratibu mzuri, alisema Waziri wa Serikali za Mitaa na Nyumba wa Zambia, Profesa Luo.

Alisema, tutaendelea kuwasiliana na nyinyi wachezaji mmoja mmoja wakati taratibu zitakapokamilika, alisema Profesa Luo.

Tayari serikali ya Zambia imeishaahidi kila mchezaji wa kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia atapewa dola 59,000 kwa ushindi wa Afrika walioupata baada ya kuilaza Ivory Coast 8-7 kwa mikwaju ya penati.

Kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na serikali ya Zambia ni kwamba dola 10,000 kwa kila mchezaji ni kwa ajili ya kufika hatua ya robo fainali, dola 13,000 kwa kufika hatua ya nusu fainali na 16,000 kwa kufika fainali na dola 20,000 kwa kutwaa ubingwa wa Afrika 2012.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine