Thursday, March 1, 2012

KAJALA: PENZI LA P FUNK HAKUNAGA








STAA wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kauli tata ya kusifia penzi la mzazi mwenzake, prodyuza Paul Mathysse ‘P Funk’ alilolitema kitambo.
Kajala alimwambia paparazi wetu kuwa vionjo vya mahaba alivyokuwa anapewa na bosi huyo wa Bongo Records, ni sawa na swaga ya Hakunaga iliyoasisiwa na msanii wa Bongo Fleva, Ismail Sadick ‘Sumalee’.
“Kusema kweli, hakunaga mwanaume niliyempenda kama P Funk, hilo siwezi kuficha,” alisema Kajala huku akifungua zaidi moyo wake kwenye akaunti yake ya mtandao wa BlackBerry Messengers (BBM) kwa kuweka ujumbe uliosomeka: “Acha waseme, nitakupenda mpaka kufa.”
Katika ujumbe huo ambao Kajala aliuambatanisha na picha mpya aliyopiga na baba wa mtoto wake huyo, uliwaweka njia panda baadhi ya marafiki zake kiasi cha wengi kuamini huenda uhusiano wa wawili hao umefufuka.



0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine