MABINGWA
wa kombe la Kagame Yanga kesho watamtambulisha rasmi beki wao wa
kimataifa Mbuyu Twite kupitia mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Coastal
Union ya Tanga utakaopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Twite
ambaye alizua gumzo baada ya kujisajili Simba na baadaye Yanga ambao
walimpandishia dau aliwasili jana na leo alianza mazoezi na wenzake
katika uwanja wa Loyola.
Msemaji
wa Yanga Lous Sendeu amesema kwamba pamoja na Twite, mashabiki wa Yanga
watapata kuwaona nyota wengine wapya waliosajuiliwa katika kikosi hicho
kwa ajili ya msimu mpya wa ligi na michuano mbalimbali.
Alisema viingilio katika m,chezo ni sh 20,000,10,000, 5,000 na 3000.
0 comments:
Post a Comment