![]() |
Simba SC |
BAADA ya mwezi na ushei wa kuwa kambini nje ya Dar es Salaam,
Alhamisi wiki hii wapenzi wa Simba SC watapata fursa ya kuiona tena timu yao
ikicheza mbele ya mechi yao, itakapomenyana na waliowahi kuwa mabingwa wa Kenya,
Sofapaka FC Uwanja wa Taifa.
Msemaji wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga ‘Mr. Liverpool’ akizungumza leo kwamba, mechi hiyo itakuwa ya mwisho kabla ya kucheza na
Azam FC, Septemba 11, mwaka huu katika mechi ya Ngao ya Jamii.
Kamwaga alisema kwamba Simba itarejea kesho Dar es Salaam na
kuendelea na mazoezi katika Uwanja wa Sigara, Chang’ombe ikisubiri kukipiga na
Azam FC.
0 comments:
Post a Comment