Mahitaji
- Kuku wa kienyeji (boiler chicken 1)
- Mchele (rice 1/2 kilo)
- Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
- Vitunguu (onion 2)
- Vitunguu swaum (garlic cloves 6)
- Tangawizi (ginger)
- Carry powder
- Binzari ya njano (Turmaric 1/2)
- Njegere(peas 1/2kikombe)
- Carrot iliyokwanguliwa 1
- Limao (lemon 1)
- Bilinganya (aubergine 1)
- Chumvi
- Pilipili (scotch bonnet pepper)
- Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Loweka mchele
kwa muda wa dakika 10 na uchuje maji yote kisha chemsha maji ya moto na uweke
pembeni. Kisha tia mafuta kiasi katika sufuria na ukaange vitunguu, carrot na
njegere pamoja. kwa muda wa dakika 5 baada ya hapo tia turmaric na chumvi. pika
kwa muda wa dakika 5 na utie mchele na maji ya moto kiasi funika na upike mpaka
uive.
Chemsha
kuku pamoja na limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi mpaka aive kisha
mweke pembeni. Saga pamoja kitunguu,kitunguu swaum, tangawizi na nyanya. Kisha
bandika jikoni na uache uchemke bila mafuta mpaka maji ya kauke.Baada ya hapo
tia chumvi, mafuta ,curry powder, bilinganya na kuku. Kaanga pamoja kwa muda
kisha tia maji au supu ya kuku kwa kukadiria mchuzi uutakao. Acha uchemke mpaka
mabilinganya yaive na hapo mchuzi utakuwa tayari kuseviwa na wali.
0 comments:
Post a Comment