Wagonjwa
wawili wameondolewa bughdha ya kutumia madawa ya kupunguza makali ya
ukimwi maishani mwao baada ya kufanyiwa upasuaji na kupandikiziwa uboho
wan binadamu au (Bone marrow), hatua inayosemekana kuondoa virusi vya
HIV mwilini mwao.
Mgonjwa
mmoja amesemekana kukaa kwa miezi minne bila ya kutumia madawa ya
kupunguza makali ya ukimwi bila ya dalili ya kurejea kwa uogonjwa huo.
Madaktai
waliofanya utafiti huo katika hospitali ya matibabu kwa wanawake ya
Brigham nchini Marekani, wanasema ni mapema mno kuzungumzia uwezekano wa
kutibu virusi hivyo kwani kuna unawezekano vinweza kurejea wakati
wowote.
Matojeo ya utafiti huo yaliwasilishwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu maswala ya Ukimwi.
Ni
vigumu sana kutibu Ukimwi, kwa sababu hujifificha ndani ya DNA,ya mtu
na hivyo kusababisha virusi sigu ambavyo haziwezi kutibika.
Madawa
ya kupunguza makali ya virusi vya HIV hudhibiti virusi hivyo ndani ya
damu lakini wakati mtu anapokosa kumeza dawa hizo, virusi hurejea.
HIV imeangamizwa?
Wanaume hao ambao hawajatajwa, wameishi na virusi hivyo kwa takriban miaka 30.
Wote walikuwa wanaugua aina ya saratani, aina ya lymphoma, ambayo ilihitaji wafanyiwe upasuaji.Seheu ya Uboho au Bone marrow ndipo celi mpya z adamu hutengezwa mwislini na inaaminika kuwa kitovu cha virusi vya HIV mwilini.
Baada ya kufanyiwa upasuaji, hapakuwa na virusi mwilini kwa miaka miwili kwa mgonjwa mmoja wakati mwingine aliishi kwa miaka minne bila ya virusi kuonekana .
Ni mapema mno kuona uoasuaji huo kama tiba ya ukiwmi na hata ikiwa itasemekana kuwa tiba basi sio tiba nzuri. Ni ghali mno na kwa baadhi ya wagonjwa kuna uwezekano wa kufariki ikiwa ni kwa asilimia15 hadi 20% kwa miaka ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji.
Wagonjwa hao sasa hawatumii tena dawa za kupunguza makali ya ukimwi. Upasuaji huu ulifanyiwa wagonjwa hao kwa sababu wlaikuwa wanaugua saratani iliyohitaji matibabu.
0 comments:
Post a Comment