Matunda yana faida nyingi mwilini na ni miongoni mwa vyakula
vinavyopaswa kupewa kipaumbele katika milo yetu ya kila siku. Lakini kwa
bahati mbaya, siyo watu wote wanaelewa umuhimu wa matunda na jinsi ya
kula ili kupata faida zake.
Kutokana na kula matunda kinyume na
utaratibu, watu wengi huyachukia matunda baada ya kujikuta wakiumwa
tumbo au kujisikia kichefuchefu na kutapika mara baada ya kula. Wengine
husikia tumbo kujaa gesi na kusikia kiungulia.
Halikadhalika, watu
wengi wamefundishwa na kuzoeshwa kulishwa matunda baada ya mlo, mazoea
ambayo ni kinyume kabisa na kanuni za ulaji sahihi wa matunda. Katika
makala haya, utaelewa njia sahihi ya kula matunda ili kupata faida zake.
KULA MATUNDA TUMBO LIKIWA TUPU
Ili
kunufaika na matunda, kula matunda wakati ukiwa na njaa na tumbo likiwa
tupu. Unapokula matunda katika hali hii, matunda husagika haraka na
virutubisho vyake husambaa mwilini kwa urahisi. Baada ya saa moja au
zaidi, unaruhusiwa kula mlo wako mwingine kama kawaida.
USILE BAADA YA KULA
Imezoeleka
na watu wengi kula matunda baada ya mlo kamili. Hata kwenye hafla na
tafrija kubwa mbalimbali, utaona matunda huliwa mwishoni baada ya
chakula. HII SIYO SAHIHI na hayo ni makosa miongoni mwa makosa mengi
yanayofanyika kwa sababu ya mazoea tu.
Inaelezwa kuwa ulaji wa
matunda baada ya mlo siyo sahihi kwa sababu matunda huyeyuka haraka
kuliko chakula cha kawaida. Tunda linapokuwa tayari kupita tumboni
kuelekea kwenye utumbo mwembamba, huzuiwa na chakula. Baada ya muda
tunda linachanganyika na chakula na kuoza na hatimaye kuzalisha asidi
ambayo humfanya mtu kuumwa tumbo baada ya kula matunda. Lakini pia
virutubisho vyake hupotea.
Ili kuepukana na hali hiyo ya
msongamano kwenye tumbo, kula matunda saa moja kabla au kama utakula
baada ya mlo, angalau kula baada ya masaa mawili. Ukila baada ya muda
huo, utakuwa umetoa nafasi ya chakula kusagika na bila kuzuia uyayukaji
wa matunda.
ZINGATIA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE MATUNDA
Baadhi
ya matunda, kama vile papai, ndizi mbivu, yana kiwango kingi cha sukari,
karibu matunda yote yana sukari, lakini mengine huwa na kiwango kingi
zaidi. Hivyo inashauriwa kula matunda kwa kiwango cha wastani kila siku
bila kuzidisha kiwango cha sukari cha gramu 25 kinachohitajika kwa siku.
Aidha,
unapokula tunda, hakikisha unakula tunda kwa ukamilifu wake ili kupata
virutubisho vyote. Kwa mfano unapokula chungwa, ni vizuri pia ukala
pampoja na nyama zake ili kupata virutubisho vyote muhimu vilivyomo.
Jiwekee
tabia ya kula matunda ya aina mbalimbali kwa nyakati tofauti ili kupata
vitamini na madini tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mwili. Kwa
kuwa matunda ndiyo yanayojenga na kuimarisha kinga ya mwili, ulaji wa
matunda ya aina mbalimbali kutakuhakikishia mwili wako kinga imara dhidi
ya maradhi na kamwe hutasumbuliwa na magonjwa mara kwa mara.
Thursday, August 22, 2013
ULAJI SAHIHI WA MATUNDA
8/22/2013 06:07:00 AM
Unknown
No comments
0 comments:
Post a Comment