PAMOJA na kuendeleza mgomo wa kutotaka kucheza soka katika kikosi cha
Etoile du Sahel cha Tunisia, bahati nyingine imemuangukia kiungo wa
zamani wa Simba, Emmanuel Okwi.
Habari za uhakika kutoka jijini Kampala zinaeleza, Ajax Cape Town, imemueleza wakala wa Okwi kwamba inataka kuimarisha kikosi chake kwa kumsajili Okwi.
“Wamesema wanamtaka aende kucheza katika kikosi chao, wanajua kuhusiana naye na wanasema walianza kumfuatilia baada ya Kaizer Chiefs kumtaka lakini mwisho ikashindikana. Tatizo moja, hapa lazima Simba walipwe fedha zao dola 300,000, hivyo kunakuwa na mzunguko. Lakini ambacho tumefanya tumewataka Ajax wazungumze na uongozi wa Etoile du Sahel kuhusiana na mchezaji huyo.
“Lakini wakati huohuo, tumewaambia hali halisi kwamba kuna ishu hii ya malipo, kuwa Etoile wanadaiwa na Simba, ingawa wao Ajax haiwahusu, lakini vizuri tu wajue,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Okwi bado yupo nchini Uganda anaendeleza mgomo wake wa kutorejea Tunisia kwa madai hawajamlipa mshahara wake tangu Februari, mwaka huu.
Hivi karibuni, uongozi wa Etoile pamoja na kusisitiza hadi Septemba watakuwa wamelipa deni hilo, lakini walijaribu kuwashawishi Simba wamchukue na kumuuza, kitu ambacho Msimbazi walikikataa.
0 comments:
Post a Comment