Tuesday, August 20, 2013

WACHUNGAJI WA DESI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3, MMOJA ACHOMOKA

Mchungaji Albogast baada ya kuachiwa huru.
Akikumbatiwa na mpendwa wake.
Wachungaji wengine wakirudishwa rumande kwa muda kusubiri hukumu.
Wakirudishwa rumande.
...Hapa wakati wakisubiri hukumu kizimbani.
Wakili wa washitakiwa, Atson Ndusyepo akiongea na wanahabari baada ya hukumu.
Umati wa watu wakiwemo waliokuwa wateja wa Desi waliofika mahakamani hapo kujua hatima ya fedha walizopanda wakitoka nje ya mahakama baada ya kuambiwa hawana chao.
Wachungaji watano wa makanisa ya Pentekoste waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuendesha biashara ya upatu kupitia Taasisi yao ya Desi Tanzania na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu leo mmoja wao aitwaye Albogast Francis ameachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia wakati wengine wanne wakihukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 21 kila mmoja pamoja na kutaifishwa mali zao.
Kesi hiyo ambayo imeunguruma kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar takribani miaka minne, kupitia kwa hakimu wake, Aloyce Katemana ilitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa utetezi na Jamhuri. Vilevile kwa wale wote waliopanda katika taasisi hiyo wote wameonekana kutenda kosa, hivyo hawana chao.

(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine