Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck
Sadiki (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Hajati Mwantum Mahiza
(kushoto) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Hajati
Mwantum Mahiza (kushoto) kwa ajili ya kuukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dar
es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa
Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni
na Michezo Barnabas Ndunguru akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja
wa wakimbiza mwenge kitaifa kabla ya Mwenge huo kukabidhiwa kwa Mkoa wa
Dar es Salaam Kulia ni Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari Assah Mwambene.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akipokea
Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa Zamda John
(Tanga) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es
Salaam.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai akitoa salamu za shukrani kwa
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajati Mwantum Mahiza (aliyevaa Miwani) kabla ya
kuukabithi Mwenge huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano
yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es
Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Kutoka
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo(kushoto)
akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa,
katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment