Thursday, September 5, 2013

BW. CHIKAMBI KARUGENDO RUMISHA ATEULIWA KUWA MSEMAJI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. M.K.Tarishi amemteua Bw. Chikambi Karugendo Rumisha (57) kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katibu Mkuu amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 6 (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 2003.
Bw. Rumisha ameitumikiwa Wizara tangu mwaka 1984 katika idara mbalimbali hali inayompa uzoefu na uelewa mkubwa wa masuala mbalimbali yanayohusu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Rumisha alikuwa akitumikia Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Sera na Mipango.
Bw. Chikambi Rumisha ambaye ni mtaalam wa elimu viumbe alihitimu Shahada ya Sayansi – Ekolojia ya Bahari na Wanyama katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1984.  
Bw. Rumisha ameitumikia Serikali katika vituo mbalimbali, pamoja na Makao Makuu ya Wizara idara ya Uvuvi alipohudumu kama Afisa Uvuvi, Kilichokuwa Chuo cha Uvuvi Nyegezi- Mwanza alipohudumu kama mkufunzi, Marine Parks alipohudumu Kama Meneja na Mwazilishi wa Taasisi hiyo na  Makao Makuu ya Wizara -Idara ya Sera na Mipango kitengo cha Ufuatiliaji .
Uteuzi huu wa Bw. C.K.Rumisha unafuatia kustafu kwa aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino ya Serikali wa Wizara, Bw. George Matiko kustaafu tangu tarehe 15/06/2013.
Bw. Chikambi K Rumisha uteuzi wake unanzia tarehe 15/8/2013 na utadumu hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Katibu Mkuu

                                            Wizara ya Maliasili na Utalii

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine