Friday, November 15, 2013

Hii ndio TV inayouzwa MILIONI 75 Mlimani City Dar es salaam, kuna picha na sifa zake pia



103
Niliwahi kuuliza kwa watu wa nguvu shilingi milioni 75 wakipata watatumia kwenye nini?, majibu ya wengi yalikua ni kujenga nyumba na kununua gari huku wengine wakisema watawekeza kwenye biashara.
Sasa basi, pamoja na hiyo milioni 75 kuonekana inaweza kufikiriwa kufanya mambo hayo makubwa ya kimaisha… imefahamika kiwango hicho cha pesa kinaweza kuishia kwenye kununua TV moja tu hii mpya ya Samsung ya inch 85 na usirudishiwe chenchi.
millardayo.com ilipotembelea duka lao Mlimani City, imeambiwa TV hii ina vitu vingi vya kipekee ikiwemo kutumia ishara ya mkono, sauti, na sura kufanya setting mbalimbali ikiwemo kupunguza sauti badala ya kutumia remote.
104
Smart contents mfano Instagram, twitter, facebook na apps nyingine mbalimbali ambapo unaweza kutumia Internet kuwasiliana kwenye mitandao mbalimbali kama vile skype ambapo mnaweza kuonana zaidi ya watu watatu kwa wakati mmoja.
Ina music system yenye mziki mzito hapohapo hivyo ukiwa nayo huna haja ya kununua home theatre, pia faster speed squad core processor.
Digital tuner unaweza kupata local free channels zaidi ya 40 bila decorder na ukitaka channel za kulipia utatumia smart card ambayo unaiweka kwenye smart card slot nyuma ya TV yako.
Vilevile ukiwa na samsung smart phone unaweza kuiunganisha na TV ukaplay videos, music video games kutoka kwenye simu yako.
105

CHANZO CHA HABARI :millardayo.com

1 comments:

Unknown said...

Kwa wale wanaopenda habari za udaku na vibwenga tembeleeni mtandao huu udaku

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine