![]() |
TOP 5 ya vipaji Miss Ilala, kutoka kushoto ni Merry Chizi, Stella Morris, Amina Sangawe, Magdalena Munisi na Mectilda Martin baada ya kutangazwa washindi jana Nyumbani Lounge. |

![]() |
Majaji kazini |




Amina Sangawe akirusha kete yake kwa majaji

Wadau wa Urembo kutoka Ukonga nao walikuwepo
![]() |
Benny Kisaka na Rutta kushoto |
![]() |
Majaji wetu, asante kwa kazi nzuri |
![]() |
Epraim Kibonde na mnazi mwenzake wa Simba, Philipo |

Mrembo akionesha kipaji cha kuchora
![]() |
Kazi ya mapacha ndio hii |
![]() |
Mapacha jukwaani |
![]() |
Ubora wa kazi ni tofauti na umaarufu wa jina...Cheki Mapacha, utafikiri bendi gani sijui la DRC lenye maskani yake Ufaransa |
![]() |
Warembo wakifuatilia shindano hilo, niwarembo wa miaka ya nyuma Ilala na Kinondoni |
![]() |
Mapacha habari nyingine bwana |

![]() |
Mtangazaji mpya wa Times FM 100.5 Gadan G, ukipenda muite Kapteni au Baba Some Food akiwa na asali wake wa moyo...Lady Jidee. upande wangu huku ni Lisa |





VIMWANA
watano usiku wa kuamkia leo wamefanikiwa kuingia fainali ya kuwania
taji la mrembo mwenye kipaji zaidi katika shindano la Miss Ilala 2012,
lililofanyika kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es
Salaam.
Vimwana
hao ni Merry Chizi, Stella Morris, Amina Sangawe, Magdalena Munisi na
Mectilda Martin, ambao waliwapiku wasichana wenzao wengine wanane,
Suzan Deodatus, Whitness Michael, na Elizaberth Pertty, Wilmina Mvungi,
Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Noela Michael na Phillios
Lemi.
Mshindi wa taji hilo, atatajwa katika kilele cha shindano la Miss Ilala 2012 kwenye ukumbi huo huo, Septemba 7, mwaka huu.
Shindano hilo lililoanza saa 2;00 usiku, lilipambwa na burudani ya bendi ya mapacha watatu na mastaa kibao wa bongo walikuwepo.
Warembo
hao, wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya wakufunzi,
Slyvia Mashuda ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008 na Miss
Ilala wa mwaka huo, na Neema Mbuya na Dickson Daudi wa THT katika
shoo.
Miss
Ilala, yenye rekodi ya kutoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss
Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe
aka K-Lyne), 2002 (Angela Damas Mutalimwa) na Salha Israel anayeshikilia
taji hilo kwa sasa, imepania kuendeleza rekodi yake nzuri mwaka huu.
Miss Ilala inahusisha warembo kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga.
SOURCE: http://bongostaz.blogspot.com/
SOURCE: http://bongostaz.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment