![]() |
Ulimwengu |
THOMAS
Emmanuel Ulimwengu, mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, akicheza mechi
yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana akitokea benchi kwenda
kuchukua nafasi ya Kanda katika kikosi cha Tout Puissant Mazembe,
alionyesha soka safi na kuitia misukosuko mno safu ya ulinzi ya Ahly,
iliyolala 2-0.
Katika
mchezo huo, mshambuliaji mwingine Mtanzania, Mbwana Ally Samatta
alifunga bao moja kwenye wa TP Mazembe mjini Lubumbashi, mechi ya Kundi
B, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Samatta
alifunga bao hilo dakika ya 49, baada ya pasi nzuri ya Tressor Mabi
Mputu, kabla ya D. Kanda kufunga la pili dakika ya 61, pasi ya Mputu
tena. Thomas Ulimwengu aliingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Kanda.
Mbwana
ni mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Mazembe kwa mwaka wa pili
sasa, lakini Ulimwengu alipandishwa kikosi hicho kwa mara ya kwanza
mwezi uliopita, baada ya kukaa kikosi cha wachezaji wa akiba tangu
asajiliwe katikati ya mwaka jana na jana amecheza mechi ya kwanza.
Mazembe
imefikisha pointi10 na kujihakikishia kutinga Nusu Fainali ya michuano
hiyo, baada ya kucheza mechi tano, kushinda tatu, sare moja na Berekum
Chelsea na kufungwa moja na Al Ahly ugenini,
Al
Ahly iliyotoa sare ya 1-1 na Berekum Chelsea nchini Ghana katika mechi
yake iliyopita, ina pointi 10 pia, wakati wababe wapya wa Ghana
wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao sita baada ya jana kutoka sare
ya 1-1 na Zamalek, ambayo inashika mkia kwa pointi yake moja.
Sasa
Ahly na TPM zitawania uongozi wa kundi hilo, ili kukwepa kukutana na
Esperance ya Tunisia inayoongoza Kundi A. Katika mechi za mwisho za
Kundi hilo, Ahly watamaliza na Zamalek mjini Cairo na Mazembe watamaliza
na Berekum Chelsea nchini Ghana.
0 comments:
Post a Comment