Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akishiriki usafi wa mazingira katika Mtaa wa Mlalakuwa na wakazi wa Mtaa huo wakati wa operesheni maalum ya kuweka safi mazingira.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa, Abraham Shoo (kushoto) wakati wa operesheni maalum ya kusafisha mazingira katika Kata za Manispaa hiyom Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Nicodemus Masika.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa tatu kushoto) akiongozana na watendaji na wakazi wa Mtaa wa Mikocheni B wakati wa opresheni ya usafi katika Kata hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni akioneshwa sehemu mbalimbali za Mto Mlalakuwa wakati wakiufanyia usafi.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni akiongozana na wakazi wa Mtaa wa Mikocheni B, katika bonde la Mto Mlalakuwa wakati wakifanyia usafi mto huo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwa kwenye picha ya pamoja na wakazi wa Kata ya Mikocheni B baada ya kumaliza kufanya usafi katika mto Mlalakuwa.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kulia) akikabidhi viroba kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni B, Sixbert Thomas kwa ajili ya kuzuia maporomoko ya ardhi katika Mto Mlalakuwa, wakati wa operesheni hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa, Abraham Shoo (kushoto) wakati wa operesheni maalum ya kusafisha mazingira katika Kata za Manispaa hiyom Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Nicodemus Masika.
………………………………………………………………………………
Na Fadhili Akida,
MPANGO wa kuweka safi mazingira ya jiji la Dar es Salaam utafanikiwa tu iwapo viongozi na watendaji watatekeleza mpango huo kwa vitendo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa operesheni maalum ya kusafisha maeneo mbalimbali ya Kata ya Mikocheni, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema umefika wakati sasa viongozi kchukua hatua za makusudi za kuhakikisha mkakati wa kuweka safi jiji unafanikiwa kwa kuwashirikisha wananchi wao kwa vitendo.
Mwenda alithibitisha hilo kwa vitendo wakati alipojumuika na wananchi mbalimbali wa Mtaa wa Mikocheni B, Manispaa ya Kinondoni kusafisha maeneo mbalimbali ya Mtaa huo ikiwemo sehemu za mto Mlalakuwa na kuwahakikishia wananchi wake kuwa hilo litakuwa zoezi endelevu ili kuhakikisha kila mwananchi anahamasika na kuweka safi mazingira yanayomzunguka.
“Kinondoni imekuwa Manispaa ya kuigwa katika suala la usafi, na hili tunalitekeleza kwa kujumuika na wananchi wenzangu kwa ajili ya kusafisha maeneo mbalimbali na leo tupo Kata ya Mikocheni B. viongozi wanatakiwa waoneshe wananchi wao kwa vitendo, nao watahamasika .” alisema Mwenda.
Meya huyo alilishukuru shirika la Kimataifa la misaada la Ujerumani (Giz) kwa kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa Manispaa yake na kuwataka wananchi waendeleze moyo waliokuwa nao ili kuhakikisha Manispaa hiyo inaendelea kuwa katika hali yake ya usafi kila siku.
Hata hivyo alitoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya ubinafsi wa kuzuia maji kufuata mikondo yake kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo watasababisha maji hayo kwenda kwa wengine na kuleta mafuriko.
Kwa upande wao wananchi wa Kata hiyo walisema wamehamasika na zoezi hilo na watahakikisha linakuwa endelevu na kutoa wito kwa wengine kuwaunga mkono na kujumuika nao wakati wa opresheni hizo.
“Operesheni ni nzuri, imetuhamasisha, tunatoa wito kwa wenzetu wengine wanaojifungia milango kujumuika na sisi kwani usafi unamuhusu kila mmoja wetu. Ukiishi katika mazingira safi hutaugua maradhi ya mara kwa mara na utafanya shughuli zako ukiwa na afya nzuri. Walisema wakazi hao.